Mgunda: Ntibazonkiza atatuvusha CAF

KOCHA msaidizi wa Simba, Juma Mgunda amesema uwepo wa Saido Ntibazonkiza unampa uhakika wa kuvuna pointi tatu katika mchezo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca utakaopigwa Jumamosi hii.

Akizungumza na HabariLEO, kocha huyo ameeleza kuwa hiyo ni kutokana na uzoefu mkubwa aliokuwa nao mchezaji huyo katika mashindano hayo makubwa.

“Nimchezo mgumu kutokana na rekodi ya wapinzani wetu kwenye mashindano haya lakini tunaini letu kubwa lipo kwa Saido sababu kwenye kikosi chetu yeye ndio mchezaji mwenye uzoefu mkubwa kuwazidi wengine hata mchezo uliopita dhidi ya Horoya AC kama angekuwepo tunaamini angefanya jambo,” amesema Mgunda.

Simba inayoshika nafasi kwenye Kundi C, Jumamosi hii itakuwa nyumbani uwanja wa Benjamin Mkapa kucheza na Raja Casablanca ambao tayari wametua nchini leo

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x