Mgunda: Simba bora inakuja

KOCHA Msaidizi wa Simba, Juma Mgunda amewaomba mashabiki wao kuwa wavumilivu kipindi hiki ambacho timu yao inapitia wakati mgumu, huku akiwasisitiza kuwa msimu ujao watarekebisha makosa yao.

Akizungumza na HabariLEO, kocha huyo amesema kuendelea kuwazomea wachezaji hakutobadilisha kile kilichowatokea, ispokuwa wanapaswa kuchukua nafasi yao kama mchezaji wa 12, ili waweze kufanya vizuri kwenye mechi zao tatu zilizosalia kabla ya kujipanga upya kwa msimu ujao.

“Kilichotokea siyo bahati mbaya, Simba siyo timu ya kwanza kukutana nacho, kitu cha msingi tunapaswa kusahau yaliyopita na tuweke nguvu kwenye mechi tatu zilizobaki kwenye ligi, ili baada ya msimu kumalizika tukajipange upya, kwa sababu zomeazomea haitabadili kilichotokea,” amesema Mgunda.

Simba Ijumaa wiki hii itashuka kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi, Dar es Salaam kucheza na Ruvu Shooting mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Habari Zifananazo

Back to top button