Mgunda: Tumpe muda Robertinho ajenge timu

KOCHA Msaidizi wa Simba, Juma Mgunda amewataka mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kumpa muda kocha wao Roberto Oliveira ‘Robertinho’, ili aweze kujenga timu imara ya mataji.

Akizungumza na HabariLEO, kocha huyo ameeleza kuwa kitendo cha kuanza kumkosoa ikiwa ndio kwanza ameanza kufanya majukumu yake ni kumfanya aone ugumu katika kazi yake mpya.

“Robertinho ni kocha mzuri ameonesha hivyo tangu akiwa Uganda, hivyo tunapaswa kumpa muda ukizingatia amekuja kwenye timu mpya na mazingira ni tofauti na alikotoka tunapaswa kumpa muda,” amesema Mgunda.

Baadhi ya mashabiki wa Simba, walionesha kutofurahishwa na kocha huyo baada ya kumfanyia mabadiliko kiungo mchezeshaji wa timu hiyo Clatous Chama kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City ambao ulimalizika kwa Simba kushinda mabao 3-2.

 

Habari Zifananazo

Back to top button