Mguu sawa ajira 25,000 afya, elimu nchini

SIMIYU: WAZIRI wa Nchi, Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa amesema mwezi ujao serikali inatarajiwa kutangaza nafasi za kazi 25,000 kwenye sekta ya afya na elimu ili kukabiliana na upungufu wa watumishi uliopo.

Pia amewataka watendaji na watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kutokubali serikali kutukanwa. Mchengerwa ameyasema hayo jana mjini Simiyu wakati wa ziara yake ya kukagua miradi na kuzungumza na watumishi mkoani Simiyu. Alisema baada ya kukamilisha taratibu za serikali, mkoa huo utaongezewa watumishi walioombwa kwenye kada mbalimbali ikiwamo za afya na elimu.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk Yahaya Nawanda alisema mahitaji ya watumishi kwa mkoa na wilaya zake ni 21,000 na waliopo ni 12,000, hivyo kuwa na upungufu wa watumishi 8,000 na kuiomba serikali kuwaondolea changamoto hiyo hususani katika sekta ya elimu na afya.

“Ukipata nafasi ishikilie kama hamuamini angalieni tuliokuwa nao serikalini huko nje hali zao zikoje, mkiweka kipimo hicho mtajiongeza kuwa kuna uhitaji wa kuwahudumia Watanzania wenye nchi yao, asije pale ukamfokea ukashindwa kumhudumia,” alisema.

Alisema katika kanzidata ya Ofisi ya Rais-Tamisemi kuna watu wanaoomba kazi kwenye sekta ya afya zaidi ya 100,000 na kwenye elimu ni hivyo hivyo.

Habari Zifananazo

Back to top button