MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amesema kinachowaponza madiwani na wabunge ni kujiita waheshimiwa.
Kinana ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara mkoani Tabora ambapo alishangazwa na madiwani kujiita waheshimiwa wakati hata mishahara hawana.
“Madiwani wanalipwa posho tu hawana mishahara kwa sababu wanaojiita waheshimiwa basi mtu ana shida yake binafsi anaenda kwa diwani ampe hela, anauguliwa diwani ndio atoe pesa ya matibabu, anasafari zake binafsi diwani ndio atoe pesa, akisema hana nongwa, tutakukata 2025.
“Wabunge wetu ndio wanaolipwa mshahara mdogo kuliko wabunge wote wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Congo, Kenya, Uganda, Rwanda ukicheki mishahara ya wabunge Iko juu kuliko wabunge wetu wa Tanzania na tukisema tuwaongeze mtasikia kelele zake.
“Wabunge wakirudi jimboni kila mtu hodi anataka apewe hela, wakati mwingine mtu anafunga safari nauliza hana mbunge ndio ampe, akasema hana nongwa, 2025 tunakutoa, si sawa hata kidogo.
“Kama Mbunge anafanya vizuri, anawaletea maendeleo, barabara, huduma za afya, shule, maji kwa nini mumtoe,hakuna haja kubadilisha wabunge kama mashati, awamu hii uyu, awamu ijayo yule..
Akitolea mfano, Kinana amesema Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya alipokua mbunge wa Same, alipeleka Maendeleo makubwa jimboni kwake kwa vile wananchi wa same walimuamini na kumuacha vipindi virefu kuwaongoza kwa kuwa mbunge wao.
“Ukienda upareni kuna milima kama nini unajiuliza kwenye Ile milima nitafikaje?
lakini cha kushangaza kuna barabara za laminate, mpaka huko milimani ni kwa nini kwa sababu mbunge amekaa vipindi virefu akafanya maendeleo. ” Amesisitiza.
Comments are closed.