Miaka 10 mafanikio ndaki ya Insia UDSM

UPANUZI wa Program zinazokidhi mahitaji ya sasa katika Ndaki ya Insia iliyopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ni miongoni mwa mafanikio yanayopatikana katika elimu.

Mafanikio hayo yanapatikana ndaki hiyo ikiwa imetimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake.

Miongoni mwa program zilizopo katika ndaki hiyo ambazo zinakidhi mahitaji ya sasa ni pamoja na cheti cha Tafsiri ya Lugha ya Alama.

“Ndaki ina Program 18 za shahada za awali na 21 za shahada za uzamili, pamoja na mbili za ngazi ya stashahada na astashahada. Mojawapo ikiwa ni cheti cha tafsiri ya lugha ya alama,” anasema Profesa Gastor Mapunda.

Profesa Mapunda amekuwa Mwenyekiti katika Kongamano la Kwanza la Kimataifa la Insia la Afrika 2023 lililofanyika Septemba 13 hadi 15 mwaka huu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Anasema kupitia watumishi wake ndaki hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa katika mfumo wa elimu nchini na kitaendelea kufanya hivyo.

Kuhusu program ya tafsiri ya lugha ya alama, Profesa Mapunda anasema ilianzishwa katika chuo hicho kama jitihada za kuwatambua wakalimani wa lugha za alama nchini.

“Astashahada ya lugha ya alama tumeanzisha kwa sababu hapa nchini wapo wakalimani wengi lakini hakuna namna ya kuwatambua .

“Hii ni jitihada ya kwanza ya kuwatambua hao wenye hayo maarifa. Maandalinzi yalianza mwaka 2014 na kufundisha tulianza rasmi 2017 kwa kushirikiana na Chama cha Viziwi Tanzania (Chavita). Ni programu ya kimkakati,” anasema.

Anasema hao wakalimani wenye utaalam huo ambao walikuwa hawajapata mafunzo rasmi wamesaidia kwa wenye matatizo ya usikivu, kwa kuwa wengi wao wanayo maarifa ila sio rasmi.

“Lugha ya alama ya Tanzania inayofundishwa chuoni hapa inachakata alama mbalimbali kutoka mikoa mbalimbali na maeneo mbalimbali Tanzania ili iwe moja.

“Alama zimewekwa pamoja sasa wanafundishwa lugha moja hivyo upotoshaji hautakuwepo tena. Tunarasimisha ili kama kuna ugumu wanapata iweze kuwa rahisi,” anasema.

Hivyo Profesa Mapunda anasema katika kutekeleza jukumu mojawapo la ubadilishanaji maarifa katika chuo hicho, ndaki hiyo imeweza kuandaa kongamano hilo ambalo ni la kitaaluma linalowakutanisha pamoja wasomi, watafiti na watendaji kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo vyuo vikuu, mabaraza ya insia, viwanda na umma kutoka ndani na nje ya ukanda wa Afrika.

Naye Rasi wa Ndaki ya Insia Dk Rose Upor anasema,” Ninapozungumzia taaluma za kiinsia nazungumzia taaluma za falsafa na dini, nazungumzia lugha, nazungumzia isimu, turathi na malikale, historia, fasihi ya lugha pamoja na historia hizo ni taaluma ambazo zimejikita ndani ya ndaki ya insia,” anasema.

Upor anasema ndaki inakutana na wasomi kusherehekea utafiti wa Insia ili kushauriana na uwakilishi mpana wa jumuiya ya wanadamu na kupanga mustakabali wa wana Afrika.

“Nimefurahishwa kwamba kwa malengo haya ya makusudi ukuaji wa Binadamu katika bara hautakuwa wa kawaida,” anasema Dk Upor tunajikita katika kuhakikisha kuwa mambo yote yanayofanyika yana ubinadamu ndani yake.

Chuo cha Insia cha UDSM kilianzishwa Oktoba 2013 baada ya kukitenganisha Chuo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii.

Anasema wanajivunia kuwa nguzo ya utafiti katika insia na kuwa chachu ya nembo ya masomo ya maendeleo ya kijamii na kitamaduni nchini Tanzania.

Anasema wanapofanya shughuli za kitafiti za kila siku hawawezi kujizuia kuona kwamba taaluma zinapanuka kwa kasi katika nchi za Magharibi na inazua swali ni nini mustakabali wetu kama wasomi wa kimataifa.

“Sisi kama Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tunataka kushiriki kikamilifu katika mazungumzo ya mustakabali wa insia ili tuje kuwa na kizazi chanye kujua umuhimu ya insia.

Ubinadamu ni muhimu katika kuelewa njia ya maisha kwa kila mwanadamu, hivyo lazima wasomi wachukue fursa ya kuunda maisha ya baadaye ya binadamu.

“Tunajivunia msaada tunaopata kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika nyanja zote na ndiyo maana tuko hapa leo kusherehekea Ubinadamu kwa Ukuaji Jumuishi,” alisema Dr Upor.

Anasema kuwa na upungufu wa ruzuku na fedha za kufanya tafiti zinapaswa kuwa ni jambo la kale. Alisema “Afrika kama bara ndilo lililoathiriwa zaidi lakini kwa ujasiri wa wasomi wa Kiafrika, tunapata sababu ya kuvumilia na hivyo kuweza kutafuta chanzo kingine cha kuendesha tafiti zetu”.

Anasema kama Afrika wanasimama kwenye jukwaa la utajiri wa kitamaduni kupitia Sanaa na pia kutafuta kwa kina chimbuko ili kujua hadithi za mababu zao na ulimwengu kabla ya wakati wao na kusimama katika kuta za makumbusho ili kuhifadhi urithi wa waafrika.

“Sisi wasomi wa insia tumejitolea katika kutafuta maarifa. Tukiwaona ninyi nyote hapa leo, inadhihirisha kwa uwazi roho ya kizalendo ya ustahimilivu kwani bila ubinadamu tunaweza kupoteza thamani za ubinadamu wetu,” anasema.

Naibu Makamu Mkuu wa UDSM upande wa taaluma, Profesa Bonaventure Rutinwa anasema insia ni mambo ya binadamu zaidi inaangalia kuanzia uchumi, siasa, jinsia na maendeleo kwa ujumla.

Na kwamba chuo hicho kinajivunia kuwa na ndaki hiyo.

“Ninaamini kwa dhati kwamba kuchukua mtazamo mpana wa kibinadamu na kimataifa kuhusu masuala ambayo yanaukabili ulimwengu wa leo ni njia muhimu ya kuwatayarisha wanafunzi na watafiti kwa mustakabali mgumu na tata, wenye masuala, wasiwasi na fursa ambazo hazijawahi kushuhudiwa,” anasema.

Anasema ili kuweza kushughulikia mahitaji ya jamii na jumuiya zake kwa siku zijazo unahitajika muunganisho na uelewa wa kina.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Garages&ServiceStations
Garages&ServiceStations
1 month ago

PATA HUDUMA YA MATENGENEZO YA MAGARI KWA MATATIZO YOTE GARI YAKO NA POPOTE ULIPO TANZANIA

NA

MOVABLE KURASINI GARAGE SERVICE STATION

Address: Dar Es Salaam,

,Post Office box: 21493,

Phone number:

022 285 1500

Categories: Garages & Service Stations.

file:///C:/Users/User/AppData/Local/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image001.jpg

– PIGA SIMU TUKUHUDUMIE

Garages&ServiceStations
Garages&ServiceStations
1 month ago

PATA HUDUMA YA MATENGENEZO YA MAGARI KWA MATATIZO YOTE GARI YAKO NA POPOTE ULIPO TANZANIA

NA

MOVABLE KURASINI GARAGE SERVICE STATION

Address: Dar Es Salaam,

,Post Office box: 21493,

Phone number:

022 285 1500

Categories: Garages & Service Stations..

file:///C:/Users/User/AppData/Local/Temp/msohtmlclip1/01/clip_image001.jpg

– PIGA SIMU TUKUHUDUMIE

Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x