Miaka 20 jela uhujumu miundombinu ya gesi

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mtwara imewahukumu kifungo cha miaka 20 jela kila mmoja washitakiwa wawili kwa kosa la kuondoa miundombinu ya gesi asilia yenye thamani ya Sh milioni 99.3 ambayo ni mali ya Shirika la Maendeleo ya Petrol nchini (TPDC).

Waliohukumiwa kifungo hiko ni Milele Masatu na Ally Danken ambao wote ni wakazi wa kijiji cha Mpapura Wilaya ya Mtwara, mkoani hapa.

Katika kesi hiyo namba 3 ya mwaka 2022 ilikuwa inawakabili watuhumiwa wanne ambao ni viongozi wa kijiji cha Mpapura, kati yao akiwepo kaimu mtendaji wa kijiji hicho imesikilizwa kwa kwa kipindi cha mwaka mmoja na kusomwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Mtwara, Lucas Jang’andu.

Kabla ya kutajwa kwa hukumu hiyo mahakama ilijiridhisha na makosa matatu yanayowakabili watuhumiwa hao na kueleza kuwa katika makosa hayo kosa namba mbili na la tatu mahakama inatilia mashaka uhasilia wa thamani ya miundombinu hiyo na kutofautiana na ripoti ya TPDC ambayo ndiyo walalamikaji.

Katokana na uthibitisho huo mahakama imewaachia huru watuhumiwa wawili ambao ni Shafii Kuchoka Kaimu Mtendaji wa kijiji cha Mpapura na Theofrid Nawesi wakati watuhumiwa namba I na 2 wametiwa hatiani na kutumikia kifungo cha miaka 20 jela.

Mahakama hiyo imewaambia watuhumiwa hao wapo uhuru kukata rufaa endapo hawatoridhika na hukumu hiyo kwa kufuata utaratibu.katika kesi hiyo upande wa Jamhuri ulikuwa na mashahidi sita.

Habari Zifananazo

Back to top button