Miaka 50 ya Hip hop na vita ya dawa za kulevya, vurugu

WAHAFIDHINA wa tamaduni ya hip hop ‘Hip Hop Culture’, leo wanaadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa utamaduni huo.

Inaaminika utamaduni wa hip hop ulianzishwa katika mji wa Bronx, New York nchini Marekani mnamo Agosti 11, 1973 kupitia Wamarekani Weusi wa mji huo.

Utamaduni huo ulianzishwa kwa lengo la kupinga na kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya pia kupambana dhidi ya vitendo vya vurugu na uvunjifu wa amani miongoni mwa Wamarekani Weusi ‘Black Americans’.

Advertisement

Kwa asilimia kubwa hip hop sasa imejipambanua kuwa chanzo cha ajira kwa vijana wengi wenye talanta na vipawa, hali iliyowaibua wafanyabiashara kadha wa kadha kuwekeza katika tamaduni hiyo.

Utamaduni huo umejengwa na nguzo au misingi mikuu minne (Four Elements) ambayo ndani yake huvunjwa vunjwa na kupata misingi saba ya hip hop.

Misingi hiyo hujumuisha i. Uimbaji wa mashairi yenye jumbe za kufundisha na kuburudisha kwa njia ya kufoka au michano pia ushereheshaji na uburudishaji wa majukwaani kwa kuzingatia tungo zenye urari wa vina na mizani ‘rapping/MCing’.

  1. Ufundi wa kusugua santuli ‘CD disk’ za miziki au kuchanganya ala za miziki na midundo katika namna ya kuburudisha wasikilizaji ‘DJing’

iii. Mtindo wa kucheza kwa njia ya kuvujavunja viungo vya mwili kwa madoido “break dancing’ na

  1. Sanaa ya kuwasilisha jumbe kupitia michoro ya sehemu za wazi ikiwemo kwenye majengo marefu, kuta pia kwenye vitambaa ‘graffiti art’

Katika nguzo zote hizo, nguzo iliyojipambanua zaidi na kuwakilisha utamaduni huo ni kupitia muziki wake ‘rapping’ ambapo umeitangaza tamaduni hiyo ndani Marekani, maeneo jirani hadi kote ulimwenguni.

Miongoni mwa wanamuziki maarufu wa rapping ulimwenguni ni pamoja na Nas, Notorious BIG, Ice Cube, Ja rule, The Game, 2 pac, 50 Cent, Eminem, Dr Dre, Suge Knight na wengine wengi.

Hata hivyo DJ Kool Herc aliyehamia New York kutokea Jamaica anatajwa kuwa ni muanzilishi wa utamaduni huo sambamba na Afika Bambaataa, Grand Master Flash na Melle Mel.

*Imeandikwa kwa msaada wa vyanzo mbalimbali kwenye mtandao.

5 comments

Comments are closed.