Miaka mitatu ya Samia heshima Sekta ya Madini

DAR ES SALAAM: Sekta ya Madini imetajwa kukua kwa kasi ndani ya miaka mitatu ya Rais Samia huku ikichangia asilimia 1 ya pato la taifa.

Hayo yamesemwa leo Machi 27, 2024 na Naibu Waziri wa Madini Mhandisi Dk Steven Kiruswa akielezea mafanikio ya wizara hiyo katika kilele cha  kurasa 365 za Rais Samia.

Dk Kiruswa amesema Sekta ya Madini kasi ya ukuaji imeongezeka na imetafsiri malengo ya taifa yaliyowekwa kwenye Dira ya Taifa ya Mwaka 2025 ambapo inaitaka sekta hiyo  kuchangia asilimia 10 kwenye pato la taifa ifikapo 2025.

“Nina furahi kusema kwamba sisi kama Wizara ya Madini chini ya uongozi wa  Rais Samia  tunakaribia kufikia lengo hilo kabla ya mwaka kesho,” amesema na kuongeza

” Kama mlivyoona wenyewe kufikia mwaka jana mahesabu yalipofungwa tulishafikia asilimia 9.1 mhandisi,”amesema.

Aidha, amesema sekta ya madini inafungamanishwa na sekta nyingine za maendeleo, hivyo serikali inatambua umuhimu wa  kuendeleza miundombinu muhimu wezeshi  ili iweze kuwezesha maendeleo kwenye tija.

Habari Zifananazo

Back to top button