SERIKALI inakusudia kuongeza tozo ya michezo ya kubahatisha kutoka shilingi 10,000 hadi Shilingi 30,000 kwa kila mashine ya Sloti kwenye maeneo ya baa na sehemu zote za kuuzia pombe zilipofungwa mashine hizo.
Akiwasilisha makadirio ya bajeti ya serikali kwa mwaka 2023/2024 Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba amesema hatua hiyo inatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 4,738 mwaka 2023/24
Pia, amependekeza kufanyiwa marekebisho kwenye Sheria ya Michezo ya Kubahatisha kwa kuanzisha michezo ya meza isiyozidi miwili katika maeneo yenye Mashine za Sloti Arobaini (Forty Machine Site).
Amesema lengo la hatua hiyo ni kuongeza ukusanyaji wa mapato yatokanayo na michezo ya kubahatisha kutoka kwenye uendeshaji wa Mashine Arobaini za Sloti
“Hatua hii inatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 4,223 kwa mwaka wa Fedha 2023/24.”Amesema
Amesema, kuanzisha ada ya maombi ya shilingi 500,000 na ada ya leseni Kuu ya dola za Kimarekani 10,000 kwa mwaka kwenye mashine za Sloti kwenye maduka; ada ya maombi ya shilingi 500,000 na ada ya leseni Kuu ya dola za Kimarekani 10,000 kwa mwaka kwenye mashine za Sloti katika maeneo ya baa.
Amesema, lengo la hatua hiyo ni kuweka utofauti kati ya shughuli za mashine za Sloti katika maeneo ya baa ‘sehemu za kuuza pombe’, maduka na shughuli za mashine arobaini za sloti pamoja na kuwezesha ufanisi na udhibiti bora wa michezo ya kubahatisha.
“ Kupunguza kiwango cha kodi kutoka asilimia 25 hadi asilimia 18 kwenye mapato ghafi ya michezo ya kubahatisha kwenye maeneo ya uendeshaji wa Mashine Arobaini za Sloti.
”Amesema
Amesema, lengo la hatua hiyo ni kuleta usawa katika utozaji kodi katika michezo ya kubahatisha inayoshabiana