Michuano ya vijana Afrika yarindima Unguja
UNGUJA, Zanzibar: UFUNGUZI wa Mashindano ya Afrika ya mpira wa miguu kwa vijana chini ya umri wa miaka 15 ‘African Schools Football Championship 2024’ umefanyika leo katika Uwanja wa New Amaan Complex, kisiwani Unguja, Zanzibar.
Timu ya Wasichana ya Tanzania imeanza kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Morocco katika Kundi A.
Soma pia: https://www.instagram.com/p/C7LtvnruhBB/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==
Kundi B, Wasichana wa Taifa la Togo wametoshana nguvu kwa suluhu tasa ya 0-0 dhidi ya Gambia, ilhali kundi hilohilo Afrika Kusini wametoka sare ya 1-1 dhidi ya Uganda.
Upande wa wavulana, Kundi A, Tanzania wametoka suluhu ya 0-0 dhidi ya Senegal. Kundi B, Guinea wamegawa kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Benin wakati wavulana wa Afrika Kusini wameibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Libya.
Soma pia: https://habarileo.co.tz/mikakati-yaanza-kusukwa-afcon-2027/
Tanzania ni bingwa mtetezi na mwenyeji wa michuano hiyo inayoendelea tena kesho, ratiba kamili tumekuwekea hapo juu @caf_online @africanschoolsfootball @tanfootball