Midizini waongoza kwa uchafu

WILAYA ya Ubungo mkoani Dar es Salaam, imeutangaza mtaa wa Midizini, uliopo Kata ya Manzese kuwa ni kinara wa uchafu kwa toka walipozindua Kampeni ya ‘Kataa Uchafu, Safisha Pendezesha Ubungo’.

Kutokana na mtaa huo kuwa kinara wa uchafu, umekabidhiwa bendera iliyoandikwa ‘Balozi wa Uchafu’ambayo itapandishwa kesho asubuhi na kupepea kwa miezi mitatu mfululizo.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Hashim Komba ameutangaza mtaa huo wakati wa tathmini ya kampeni hiyo iliyofanyika leo, ambapo kila baada ya miezi mitatu tathmini itafanyika.

Ameitaja mitaa mingine michafu ambayo haijapewa bendera kuwa ni Kilimahewa na Kwa Jongo iliyopo kata ya Makurumla, pamoja na Muungano uliopo Kata ya Mazese.

“Mtaa umefanya vibaya Kata ya Manzese wanataka kutuletea kipindupindu, hatutaki kipindupindu. Kesho nitapandisha bendera katika mtaa huo na kuzungumza na wananchi,” amesema.

Pia ameutaja mtaa unaoongoza kwa usafi kuwa ni Kibururu Kata ya Goba, wamepewa zawadi ya sh 600,000.

Mtaa wa pili kwa usafi ni Sinza A uliopo kata ya Sinza wamepewa sh 400,000 na mtaa wa tatu kwa usafi ni Mabibo wamepewa sh 300,000

Habari Zifananazo

Back to top button