Mifumo DP World kudhibiti mianya udhibiti mianya upotevu wa mapato

KUTOKANA na madai ya kuwepo changamoto za mifumo madhubuti na kusababisha baadhi watu wasio na uadilifu kujihusisha na vitendo vya udanganyifu na kupoteza mapato ya Serikali katika Bandari ya Dar es Salaam na bandari nyingine nchini, Kampuni ya DP World (DPW) inayotarajiwa kuwekeza kwenye bandari hiyo itadhibiti vitendo hivyo kwa kusimika mifumo madhubuti ya Tehama.

Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO, Gerson Msigwa ameliambia HabariLEO kuwa DP World wataweka mifumo ambayo itadhibiti vitendo viovu katika Bandari ya Dar es Salaam.

Msigwa anasema kutokana na mpango huo wa serikali wa kutaka kuifanya Bandari ya Dar es Salaam kuwa na tija na kuvutia wafanyabiashara wengi wa ndani na nje, baadhi ya watu wenye maslahi na udhaifu wa mifumo iliyopo ya uendeshaji, wameamua kuendesha propaganda dhidi ya serikali na DP World.

“Kwa namna yoyote ile wapigaji hawawezi kuipenda Kampuni ya DP World, hii ni vita ya uchumi. Kwa mfano DP World wanakuja kujenga maghala ya kuhifadhia nafaka, kwa sasa maghala ya TPA yana uwezo wa kuhifadhi tani 30,000 tu za nafaka, lakini DP World wanataka kujenga maghala ya kuhifadhi tani milioni 30 za nafaka,” anasema Msigwa.

Anaongeza: “Kwa mfano korosho zinatarajiwa kuvunwa tani 200,000, utaziweka wapi wakati uwezo wetu ni tani 30,000, kwa hiyo hapa kuna vita kubwa ya kupinga mpango huu wa serikali, na miongoni mwa wanaopinga wanajua wanavyonufaika na udhaifu na ufanisi duni wa bandari.” Msigwa anasema DP World pia watajenga maeneo ya kuhifadhi makontena ili kuongeza ufanisi na tija ya bandari mara kumi zaidi.

Anasema DP World wamejenga bandari kavu Kigali, Rwanda yenye uwezo wa kuhifadhi makontena 50,000 na sasa wanaipanua na kutokea hapo ndio wanaihudumia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), hivyo serikali imeona vyema ikafanya kazi na kampuni hii kwa kuwa tayari ina mtandao wa kutosha wa kibiashara.

Wakati wa mjadala wa kitaifa kuhusu kulinda na kuendeleza umoja wa kitaifa wakati wa mageuzi ya kisiasa na kiuchumi uliofanyika Dar es Salaam hivi karibuni, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Angelina Ngalula alisema ana uzoefu wa miaka 20 wa kufanya shughuli za kibiashara katika Bandari ya Dar es Salaam, hivyo anaijua vizuri.

Ngalula anasema fursa ambazo Bandari ya Dar es Salaam inazikosa kwa muda mrefu sasa ni nyingi na zingeweza kubadilisha uchumi wa nchi kwa kiasi kikubwa.

“Tumekaa kama kisiwa, bandari lazima idhibiti mnyororo mzima wa usafirishaji la sivyo hatutafanya biashara, lazima idhibiti kuanzia mzigo unakotoka, ufike hapa na kisha ufike kwa mteja, sasa tunamiliki bandari lakini tunamsubiri mtu ambaye hatuna miadi naye atuletee mzigo badala ya sisi kwenda kuutafuta mzigo na kuuleta,” anasema Ngalula. Anaongeza:

“Jambo hili linamhitaji mtu ambaye ana mtandao duniani au kampuni kubwa ili atuletee mzigo, tunahitaji mtu wa kutukusanyia mizigo huko iliko atuletee ili nasi tuweze kukusanya mapato, tunamhitaji Bandari ya Dar es Salaam na kampuni hizo zinafanyakazi kwenye nchi zaidi ya 100 duniani. Katika hilo anahoji kampuni hizo zinafanyakazi na nani wa kuwaambia mizigo yao wailete Bandari ya Dar es Salaam kwa kuwa kampuni hizo moja tu inaweza kuwa na mapato yasiyopungua Dola bilioni 200.

Mkuu wa Chuo cha Bandari Dar es Salaam, Dk Lufunyo Hussein anasema sekta binafsi ina utaalamu wa uendeshaji wa shughuli za bandari unaotokana na uzoefu wa kufanya shughuli hizo katika maeneo mengi duniani.

Anasema kupitia uzoefu huo walionao pamoja na teknolojia na utaalamu, sekta binafsi ina uwezo wa kuongeza ufanisi wa utoaji huduma za bandari pale inapopewa fursa ya kufanya hivyo. Katika muktadha huo wa kushirikisha sekta binafsi kuwekeza katika bandari, Dk Lufunyo anabainisha kuwa hii siyo mara ya kwanza kwa Serikali ya Tanzania kutafuta mwekezaji katika uendelezaji na uendeshaji wa bandari.

Anasema mwaka 2000 serikali kupitia TPA ambayo kipindi hicho ilikuwa inajulikana kama Mamlaka ya Bandari Tanzania (THA) na Tume ya Rais ya kurekebisha mashirika ya umma (PSRC), iliingia mkataba na Kampuni ya kimataifa ya kuhudumia makasha (TICTS).

Dk Lufunyo anasema kampuni hiyo ya TICTS imefanya kazi kwa muda wa miaka 22 hadi kufikia mwezi Desemba mwaka jana katika gati namba 8 hadi 11 za Bandari ya Dar es Salaam.

Anasema kama sekta binafsi haitapewa nafasi katika masuala ya uendeshaji bandari, Serikali ikabaki kuendelea na utaratibu wa sasa wa uwekezaji katika miundombinu, kuendesha na kununua vifaa, basi bandari zetu zitaendelea kuwa duni na kuathiri utendaji wa bandari na kulikosesha taifa mapato.

Kwa mujibu wa Dk Lufunyo, sheria iliyoanzisha TPA inaipa mamlaka hiyo jukumu la kumiliki, kusimamia, kuendeleza na kuendesha maeneo ya bandari Tanzania Bara.

Pia anasema baadhi ya madhumuni ya kuanzishwa kwa TPA ni pamoja na kuhakikisha Tanzania inafaidika na faida ya kijiografia, kuchagiza usimamizi bora na ufungamanishi wa tija katika bandari, kuhakikisha kuna tija kwenye huduma za bandari, kuboresha na kusimamia miundombinu ya bandari, kuingia mikataba au makubaliano na mtu au taasisi ya kutoa huduma za bandari na kuhakikisha uwepo wa ulinzi na usalama wa bandari.

Kwa mantiki hiyo, Dk Lufunyo anasema ili kutatua changamoto za sasa katika bandari nchini, serikali ilipokea mapendekezo ya wawekezaji mbalimbali ikiwemo Kampuni ya Hutchson ya Hong Kong, Antewerp/Brugge (Belgium), PSA International (Singapore), DP World (Dubai), Abu Dhabi Ports (Abu Dhabi), Adani Ports and Logistics (MundraIndia), CMA-CGM (France) na Kampuni ya Maersk ya Denmark.

Pia anasema kwa kuzingatia dhima ya kutaka kuongeza tija na ufanisi katika bandari, Serikali ya Tanzania kupitia TPA imesaini Hati ya Makubaliano (MoU) na Serikali ya Dubai kupitia Kampuni ya DP World.

Dk Lufunyo anasema miongoni mwa maeneo ambayo DP World itawekeza ni eneo litakaloongeza tija na ufanisi katika utoaji wa huduma za bandari pamoja na kuimarisha mifumo ya Tehama katika huduma za kibandarimtu mwenye uwezo wa teknolojia na uwezo wa fedha kuwekeza kwenye miundombinu ili tupate tunachotarajia.” Ngalula anasema nchini DRC kuna kampuni kubwa nne ambazo zinajihusisha na asilimia 80 ya mzigo uliopo DRC ambao unapita kwenye

Habari Zifananazo

Back to top button