Mifumo salama makazini chachu ya mabadiliko
ARUSHA: NAIBU Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete amesema mabadiliko ya kweli yataletwa na mifumo salama ya kazi kwa waajiriwa, pamoja na mienendo ya kiutendaji miongoni mwa Maofisa Rasilimali Watu.
Soma pia: https://habarileo.co.tz/kikwete-mifumo-ya-pepmis-pipmis-itaondoa-uonevu/
Hayo yamesemwa na naibu waziri huyo wakati akifunga Mkutano wa 11 wa wanachama wa Chama Cha Maafisa Tawala na Rasilimali Watu (AAPAM) uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha jijini Arusha (AICC).
Ridhiwani amewataka Maafisa hao kuendelea kutumia mifumo ya utendaji kazi ili kuwezesha haki na wajibu kutolewa kwa watumishi wa umma.
Aidha, aliwakumbusha watumishi hao mifumo mbalimbali iliyokwisha tengenezwa kuwezesha watumishi kukopa, kuhama na kupima utendaji kazi.
Pia, amewaonya Maafisa hao juu ya tabia inayoendelea ya kutowatendea vyema watumishi wenzao wanaowaongoza.
Ameonya juu ya roho mbaya walizonazo baadhi ya Watendaji hao akitoa mfano wa Rorya na taratibu za upandishaji madaraja.