Mifumo ya uzazi kutengeneza damu

DAR ES SALAAM: CHUO Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) kimeanza kufanya utafiti wa kutengeneza damu kutoka kwenye mifumo ya uzazi na kutengeneza benki ya sampuli za seli na vinasaba.

Hayo yamesemwa na Mtafiti wa Idara ya Micro Chemistry na Microbiology kutoka MUHAS ambaye pia ni Mhadhiri wa chuo hicho, Dk Mohamed Zahir, katika maadhimisho ya miaka 47 ya ushirikiano kati ya chuo hicho  na Sweden kupitia Shirika la Maendelea la Sweden(SIDA) na miaka 60 ya ushirikiano kati ya Tanzania na Sweden

Dk Mohamed amesema, lengo la utafiti huo ni  kutengeneza miundombinu ambayo itawezesha kuchukua  damu kutoka kwenye mfumo wa uzazi na kutengeneza benki, kuhifadhi sampuli za seli na vinasaba ili kufanya matibabu ya masuala mbali mbali yakiwemo magonjwa ya selimundu.

“Dunia hii kuna maradhi watu wanarithi na maradhi ya kurithi mara nyingi hayana tiba sahihi, teknolojia inavyoenda tunahitaji kutumia miundombinu mipya tutumie vifaa vipya vitakavyotusaidia kupata matibabu sahihi na matibabu ambayo hawa wagonjwa wanastahili kupata.”Amesema Dk Mohamed na kuongeza

“Kwa hiyo,  tunataka kutengeneza miundombinu ya benki ya damu kutoka kwenye mfumo wa mtoto kuzaliwa kuna faida nyingi sana kwa kutumia mfumo huo kwa sababu unapata seli kwenye wagonjwa  wenye magonjwa ya kurithi.

“Tunachojaribu kufanya ni kutengeneza benki, tukipata mtu ambaye ana ugonjwa fulani na seli zake zimeharibika hazifanyi kazi inavyotakiwa  basi kwenye benki yetu tutakuwa na seli ambazo tutaweza kudoneti kwa mtoto au mama mwenye changamoto hiyo na apate matibabu sahihi ambayo anayo.”Amesisitiza

Aidha, ameishukuru SIDA na ubalozi wa Sweden kwa kutoa fedha ambazo zinasaidia  mwanasayansi kukua na kufanya tafiti ambayo Tanzania inastahiki ili kuweza kuboresha miundombinu ya nchi.

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button