Migogoro ya ardhi, Rais Samia akemea wanasiasa

Yaliyompaisha Samia 2022

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amekemea tabia ya  wanasiasa  kuchochea migogoro ya ardhi kwa mtaji wa kisiasa na kuwataka kuacha tabia hiyo mara moja.

Rais Samia ameyasema hayo leo Novemba 23, 2022 mkoani Manyara na kuwataka wanasiasa kuacha tabia ya kuwatetea wavamizi wa ardhi kwa malengo ya kisiasa.

Advertisement

“Kuna tabia kwa wanasiasa, mnakaa kimya maeneo yanapovamiwa, lakini  baadae mnasimama na kuwatetea ili kupata kura wakati wa uchaguzi, tabia hiyo si nzuri muache.”Amesema Rais Samia na kuongeza

“Unajua, wamevamia na wameharibu mipango ya matumizi bora ya ardhi, unasimama kuwatetea ili upate kura,” amesisitiza.

|Rais Samia amewataka wanasiasa hao kuacha kuchochea migogoro kwani inapoteza muda mwingi na kuchelewesha maendeleo na badala yake wasimame na serikali katika kupanga matumizi bora ya ardhi.

“Eneo ambalo wananchi wangelitumia kwa maendeleo halitumiki kwasababu lipo kwenye mgogoro hadi umalizike. Niombe sana wananasiasa tusaidiane kwenye jambo hili tusichochee migogoro,” amesisiitiza

Rais , Samia Suluhu Hassan akikemea tabia ya wanasiasa kuchochea migogoro ya ardhi