KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, John Jingu amesema kuwa migogoro ya kifamilia imekuwa ikiwawaweka watoto katika hali mbaya ya malezi na kuongeza ukatili kwa watoto.
Ameeleza kuwa kwa sasa wanashuhudia migogoro mingi ya ndoa katika familia ambapo watoto huwa ndio waathirika wakubwa huku takwimu za wizara za Julai 2022 hadi Aprili 2023 jumla ya mashauri 1,574 ya migogoro ya ndoa na familia ilipokelewa katika mabaraza ya ushuluhishi ya ndoa kutoka ngazi za Halmashauri na wizarani.
Kati ya mashauri hayo 895 yalifanyiwa usuluhishi na mashauri 679 yalipatiwa rufaa ya kwenda mahakamani.
Akizungumza leo jijini Da es Salaam katika mkutano wa viongozi wa dini na wizara hiyo, Jingu amesema kwa watoto ambao wanaishi na kufanya kazi hadi kufikia Machi, 2023 watoto walikuwa 335,971, kati yao wa kiume 168,634 na wa kike 167,337 walibainishwa kuishi katika mazingira hatarishi.
“Jumla ya watoto 2,185 kati yao wa kiume 1,324 na wa kike 861 waliokuwa wanafanya kazi na kuishi mitaani waliunganishwa na familia zao ili kuwasaidia watoto wanaoishi serikali imeratibu uanzishwaji wa Makao ya Watoto 333 ya Serikali na Binafsi ambayo yanahifhadhi watoto 12,077.
Amesema kuwa familia ina wajibu mkubwa katika kutengeneza jami hivyo wazazi na walezi wasipotimiza wajibu wao ipasavyo wa kuhakikisha kuwa malezi na makuzi ya watoto yanaendana na maadili ya jamii na inawafanya watoto wawe ni wanajamii wanaojitambua, wenye kukubalika na wenye mchango katika jamii na taifa.