Mikakati kuboresha sekta ya anga yajadiliwa

ARUSHA: Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari amewasilisha taarifa ya utendaji ya TCAA katika Mkutano wa 16 wa Tathimini ya Utekelezaji katika Uchukuzi na Usafirishaji ulioandaliwa na Wizara ya Uchukuzi unaofanyika mkoani Arusha kuanzia Desemba 5 hadi 8, 2023.
Mkutano huo wa siku nne unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), ulifunguliwa na Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa umewakutanisha wakuu wa Taasisi chini ya Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Ujenzi, TAMISEMI pamoja na wadau wa sekta ya uchukuzi kutoka sekta binafsi.
Wasilisho hilo limegusa mipango ya Taasisi, mafanikio pamoja na changamoto ambapo wadau walijadili kwa pamoja namna bora ya kuboresha utendaji ili kuboresha sekta ya usafiri wa anga nchini.
1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *