Mikakati utekelezaji wa miradi ya nishati safi ya kupikia

DAR ES SALAAM: Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dk.Selemani Jafo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Tine Tonnes.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika ofisi ndogo ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam viongozi hao wamejadili kuhusu utekelezaji wa miradi ya nishati safi ya kupikia.

Dk. Jafo amemueleza, Balozi Tinnes dhamira ya serikali katika kuimarisha upatikanaji wa nishati safi na kuachana na matumizi ya kuni na mkaa kwa kuanza na taasisi zenye kulisha idadi kubwa ya watu.

Advertisement

Amesema Serikali inaendelea kuwekeza na kuhimiza matumizi ya nishati safi ya kupikia hususan ya gesi katika shule na vyuo mbalimbali ili ziachane na matumizi ya kuni na mkaa ambayo inaonekana kuwa ni ya gharama zaidi.

Kwa upande wake Balozi Tinnes amesema kuwa dhamira ya Serikali yake ni kuwekeza katika miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi hasa katika nishati safi.

Baadhi ya miradi ambayo Balozi ameitaja ni pamoja na uwekezaji katika nishati ya baiogesi, umeme unaozalishwa na maji pamoja na usimamizi wa taka ngumu.

 

 

 

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *