Mikakati yawekwa upatikanaji dawa
SERIKALI imesema inaendelea kuboresha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika hospitali nchini kwa kutekeleza mambo mbalimbali ikiwemo kuipatia mtaji Bohari ya Dawa ili kuwa na bidhaa za afya muda wote.
Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel ametoa kauli hiyo bungeni leo, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Tabora Mjini, Emmanuel Mwakasaka aliyehoji mkakati uliopo wa kumaliza upungufu wa dawa na vifaa tiba katika hospitali nchini.
“Serikali inaendelea kuboresha upatikanaji wa madawa na vifaa tiba katika hospitali zetu nchini kwa kutekeleza yafuatayo;
“1. Kuipatia mtaji Bohari ya Dawa kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ili kuwa na bidhaa za Afya muda, 2. wote. 2. Serikali kutoa fedha za ununuzi wa bidhaa za afya kila mwezi kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za Afya vya Umma.
“ 3. Kuhakikisha suala la usimamizi wa bidhaa za afya linakuwa sehemu ya ajenda ya Kudumu ya Kamati za ulinzi na usalama za wilaya na mikoa.
“4. Kuwasimamia watoa huduma katika vituo vya kutolea huduma za afya ili kuweza kukadiria kwa usahihi. (Forecasting) 5. Vituo vya kutolea huduma za afya kutumia fedha zinazotokana na malipo ya huduma na dawa kununua bidhaa za afya kuliko kutegemea fedha zinazotolewa na Serikali pekee,” amesema Naibu Waziri Mollel.