Mikhail Gorbachev: Kiongozi aliyemaliza vita baridi afariki akiwa na miaka 91

Mikhail Gorbachev, Kiongozi wa mwisho wa Muungano wa Sovieti

Mikhail Gorbachev, Kiongozi wa mwisho wa Muungano wa Sovieti na ambaye anatajwa kumaliza Vita Baridi amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 91, vyombo vya habari vya Urusi vimeripoti vikitaja maradhi ya muda mrefu.

Gorbachev alijulikana katika duru za mwanasovieti mnamo 1985, baada ya kifo cha Brezhnev na kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa chama cha Kikomunisti. Aliamini kuwa serikali kuu na urasimu katika USSR kusaidia kukuza uchumi na ndipo alipo anzisha utaratibu wa urekebishaji na uwazi ambao uliangusha mapazia ya ukomunisti.

Wakati wa utawala wake kama kiongozi wa USSR, Gorbachev atakumbukwa kuwa mtu ambaye alikutana uso kwa uso na Rais wa Marekani Ronald Reagan katika mkutano wa kilele nchini Iceland na kutaka kukomeshwa kwa makombora yote ya masafa marefu yaliyokuwa yakishikiliwa na Marekani na Usovieti. 

Advertisement

Wawili hao walitia saini Mkataba wa Kupambana na Kueneza Nyuklia ambao ulikuwa mwanzo wa mwisho wa Vita Baridi.

Hata hivyo angejulikana kama ‘dikteta wa karatasi’ katika utawala wake wa USSR huku sera zake zikielezwa kuwa rahisi lakini si za kiutendaji, Urusi ilisambaratika mikononi mwake na alidharauliwa na kudhihakiwa nchini mwake, mapinduzi yalifanyika Agosti 1991 na hivyo kuangusha chama cha kikomunisti na Umoja wa Kisovieti mnamo Desemba 1991.

Alitunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka wa 1990 “kwa jukumu lake kuu katika mchakato wa amani ambao leo unajumuisha sehemu muhimu za jumuiya ya kimataifa.”

1 comments

Comments are closed.