Mikoa 11 hatarini tisho la Ebola

Waziri atoa taadhari

WIZARA ya Afya imetoa tahadhari ya  tishio la ugonjwa wa Ebola huku ikitaja mikoa 11 ambayo iko hatarini  kukumbwa na ugonjwa huo ambapo hadi sasa hakuna mgonjwa aliyepatikana.

Akizungumza na waadishi wa Habari leo Septemba 28,2022 jijini Dar es Salaam,Waziri wa Afya ,Ummy Mwalimu amesema mikoa iliyopo hatarini zaidi  ni Kagera, Mwanza, Kigoma, Geita na Mara.

Mikoa ya Dar es salaam, Arusha, Kilimanjaro, Songwe, Mbeya na Dodoma nayo imetajwa kuwa hatarini kwa sababu ya uwepo wa viwanja vya ndege na vituo vikubwa vya mabasi ya kutoka nchi jirani.

Waziri wa Afya ,Ummy Mwalimu akielezea tishio la Ebola nchini

Amesema serikali ilipokea taarifa Septemba 20, 2022 kutoka kwa Waziri wa Afya wa Uganda, kupitia vyombo mbalimbali vya habari juu ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika Wilaya ya Mubende nchini humo.

“Wilaya ya Mubende iko umbali wa takribani kilometa 130 hadi Kampala, Makao Makuu ya Uganda na  kutoka Kampala hadi Mutukula mkoani Kagera Tanzania ni umbali wa takribani kilometa 220,”Amesema Ummy.

Amesema hadi kufikia Septemba 26, 2022, jumla ya wagonjwa 43 na vifo 23 vimetolewa taarifa.

Ummy amesema taarifa zinaonesha kuwa dalili za watu wenye ugonjwa huo upatwa na  homa kali, degedege, kutapika matapishi yenye damu, kuharisha na kutokwa damu machoni.

“Uchunguzi wa kimaabara umethibitisha kuwepo kwa ugonjwa wa Ebola anuai aina ya Sudan (Ebola-Sudan strain) na hadi sasa jumla ya watu 425 waliotangamana na wagonjwa wameanishwa na kati yao watu 127 wamepatikana na wanafuatiliwa ikiwa wataonyesha dalili za kuwa na ugonjwa huo,”ameeleza.

 

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button