Mikoa 26 yavuka 100% chanjo ya polio

WIZARA ya Afya imesema mikoa 24 imetoa chanjo ya polio kwa zaidi ya asilimia 100. Taarifa ya Waziri wa wizara hiyo, Ummy Mwalimu jana ilieleza kuwa watoto 14,690,597 walipata chanjo hiyo ambao ni sawa na asilimia 118.6 ya malengo waliyoweka.

Ummy alisema ufanisi wa utoaji wa chanjo hiyo ulitofautiana kutoka mkoa mmoja hadi mwingine na kwa ngazi ya mikoa, Kilimanjaro imevuka lengo kwa asilimia 166.96, Katavi 129.25% na Dar es Salaam 124%.

Alitaja mikoa mingine iliyovuka asilimia 100 kuwa ni Ruvuma 122.91%, Geita 122.66%, Singida 122%, Mara 119.84%, Pwani 119.66%, Songwe 119.19%, Lindi 118.60%, Rukwa 117.75%, Dodoma 117.56% na Morogoro 117.53%.

Pia Shinyanga 116.91%, Mbeya 116.91%, Kigoma 116.68%, Tabora 116.27%, Simiyu 115.75%, Mtwara 114.93%, Tanga 114.23%, Mwanza 113.54%, Njombe 112.61%, Arusha 112.46%, Manyara 110.09%, Kagera 110.05% na Iringa 109.03%.

Ummy alisema wizara inawapongeza na kuwashukuru wakuu wa mikoa, makatibu tawala wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, wataalamu wa afya, mashirika ya kitaifa na kimataifa, vyombo vya habari na wananchi kwa kufanikisha utekelezaji wa kampeni ya awamu ya tatu ya utoaji chanjo hiyo.

Alitoa mwito wa ushirikiano katika kampeni ya awamu ya nne na ya mwisho inayotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu au tarehe nyingine itakayotangazwa baadaye.

Septemba Mosi hadi 4, mwaka huu Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) ilitekeleza awamu ya tatu ya kampeni ya chanjo ya polio ya matone dhidi ya ugonjwa wa polio nchi nzima.

Habari Zifananazo

Back to top button