‘Milango ipo wazi sekta binafsi kuwekeza’
DODOMA: SERIKALI imesema maendeleo ya nchi ni shirikishi, hivyo milango ipo wazi kwa sekta binafsi kuwekeza nchini na kufanya biashara.
“Kila pale ambapo sekta binafsi inaweza kuweka fedha na sisi serikali fedha ile tusiiweke tukaitumia kwenye mambo mengine ya maendeleo,” amesema Rais Samia.
Hayo yameelezwa na Rais Samia Suluhu Hassan leo Oktoba 22, 2023, katika hafla ya utiaji saini wa mikataba mitatu ya uendelezaji na uendeshaji wa Bandari ya Dar es Salaam, kati ya Serikali ya Tanzania chini ya Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) na Kampuni ya DP World ya nchini Dubai katika Ikulu ya Chamwino, Dodoma.
Hata hivyo, Rais amewatoa hofu Watanzania kwa kusema hakuna atakayepoteza ajira kutokana na uwekezaji huu wa DP World.
“Kama alivyosema Mkurugenzi (Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), Plasduce Mbossa) hakuna atakayepoteza kazi ima muajiriwa wa bandari hata wanaofanya kazi bandarini,” amesema Rais Samia.