Milioni 320 kuchangwa kusaidia huduma za kijamii

DAR ES SALAAM: Jumla ya wadhamini 18 wamejitokeza kudhamini uchangiaji wa gharama za masomo ya elimu ya juu nchi kwa wanafunzi 100 ambao hawana uwezo wa kulipa ada.

Wadhamini hao wamejitokeza kufanikisha mashindano ya mbio za mbuzi zilizoandaliwa na Rotary Club ya Oysterbay kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania ambayo yanatarajiwa kufanyika Septemba 9,2023 katika viwanja vya The Green Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Katika mashindano hayo zaidi ya watu 3000 wanatarajiwa kushiriki huku kiasi cha sh milioni 320 zikitarajiwa kuchangwa kwaajili ya huduma za kijamii ikiwemo elimu,afya ,miundombinu na zingine.

Advertisement

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam,Meneja Masoko wa YARA Tanzania, Salha Mwerema amesema wao wamekuwa wakijihusisha na utoaji wa mbolea ambapo pia wamekuwa wakiwasaidia wanawake na vijana kuweza kufanikisha kilimo cha kisasa.

“Mwaka huu tunashiriki mbio za mbuzi kutokana na malengo yaliyowekwa
Sisi kama kampuni tunatoa mchango kusaidia vijana na wanawake katika kufanikisha kilimo na hivyo tumeona malengo yetu yanafanana hivyo tutakwepo kushirikiana na Rotary kufanikisha.

Amesema wameona ni muda mwafaka sasa wa kurudisha hisani kwa jamii kwa njia hiyo licha pia kushiriki kwa njia nyingine.

Kwa upande wake Meneja wa Vodacom Tanzania, Sandra Oswald amesema wameona kuna umuhimu wa kuunga mkono jitihada za kuweza kuratibu mashindano ya mbio ya mbuzi ili kusaidia ufadhili kwa wanafunzi wa elimu ya juu na kusaidia shughuli za kijamii.

“Tunadhamini sana hili kama wadau wa maendeleo na tunashukuru Rotary Club ya Oysterbay ambapo sh milioni 320 zitakusanywa tumeona ni vyema kuungana kama chachu ya maendeleo,”amesisitiza.

Meneja Mradi wa mbio hizo Paul Muhato amesema Vipaumbele vya mwaka huu vitakua katika jitihada za kuwezesha, kupanua, na kutangaza miradi ya kijamii ambayo itahusisha miradi mipya, pamoja na miradi mengine inayo endelea kama vile misaada ya elimu, utoaji vifaa na elimu ya usafi, amani na usuluhishi wa migogoro, kujikinga na kutibu maradhi, maji na usafi, afya kwa waja wazito na watoto, elimu ya msingi, uchumi na maendeleo ya jamii.

3 comments

Comments are closed.