Milioni 48 Afrika wakabiliwa na uhaba wa chakula

WATU milioni 48 barani Afrika wanakabiliwa na uhaba wa chakula hali iliyosababishwa na hali ya hewa, ukosefu wa usalama na magonjwa huku watu 130,000 wakiwa na hali mbaya ya kupoteza maisha. Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) limesema.

Imeelezwa Dola milioni 178 zinatakiwa ili kutoa msaada kibinadamu katika nchi saba zilizoathiriwa katika eneo la Greater Horn. Mfanyakazi mkongwe wa WHO Liesbeth Aelbrecht alionya kwamba hali ni mbaya zaidi kuliko miongo miwili huko Djibouti, Ethiopia, Kenya. Somalia, Sudan Kusini, Sudan na Uganda.

“Watu hawa milioni 48 ni pamoja na 129,000 ambao wanakabiliwa na janga na maafa, hiyo inamaanisha wanakabiliwa na njaa na kifo machoni,” Bi. Aelbrecht aliwaambia waandishi wa habari mjini Geneva.

Advertisement

Alisema watu ambao wako hatarini zaidi ni kutoka Sudan Kusini na Somalia.

Mbali na janga la njaa, eneo hilo halijawahi kuona idadi kubwa kama hii ya milipuko ya magonjwa iliyoripotiwa, WHO imeeleza. “Nchi zote saba zinapambana na surua, ugonjwa hatari,” Bi. Aelbrecht alisema.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *