Minziro ataja sababu nyota Geita kuchukuliwa

KOCHA Mkuu wa Geita Gold, Fredy Minziro, amesema sababu ya timu nyingi kukimbilia kuwasajili wachezaji wao kwenye dirisha dogo ni kutokana na kuwajengea uwezo mkubwa wa kucheza soka la ushindani.

Akizungumza na HabariLEO, kocha huyo ameeleza kuwa ingawa inamrudisha nyuma katika timu, lakini hakuna namna sababu mpira ni biashara nzuri na huu ndio msimu wake.

“Ni kweli inarudisha nyuma maendeleo ya timu, lakini tukumbuke hii ni biashara pia na kwangu kama kocha CV yangu inakua kwa kumjenga mchezaji huyo mpaka kuuzwa kiasi kikubwa cha pesa tofauti na tulipomsajili,” amesema Minziro.

Tangu dirisha dogo la usajili lifunguliwe Desemba 16, Geita GoldĀ  FC imeshaondokewa na wachezaji sita wakijiunga na timu nyingine wachezaji hao ni Saido Ntibazonkiza, Yusufu Kagoma, Adeyum Salehe, George Mpole, Kelvin Nashon na James Msuva.

Habari Zifananazo

Back to top button