Minziro: Tupo tayari kumkabili Simba

MBEYA: Kocha wa Tanzania Prisons Fred Felix Minziro amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi Oktoba 5, 2023 katika dimba la Sokoine jijini Mbeya watakaposhuka dimbani kuivaa Simba kwenye mchezo wa ligi kuu bara.
Kocha huyo amesema wamejiandaa vya kutosha kuelekea mchezo huo muhimu wa siku ya kesho na tayari wamaefanyia kazi makosa yaliyojitokeza kwenye michezo iliyopita na wapo tayari kuwapa furaha mashabiki wa timu hiyo.
Amesema mashabiki Prisons wanapaswa kujitokeza kwa wingi kuipa nguvu timu yao ili kupata matokeo mazuri.

Ikumbukwe Prisons bado hawajaonja ladha ya ushindi kwenye ligi msimu huu wakiwa wameshuka dimbani mara tatu, wakipokea vipigo kwenye michezo miwili huku wakiambulia sare katika mchezo mmoja, na wanaburuza mkia kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama moja.

Habari Zifananazo

Back to top button