Miradi 135 ya utafiti yafanyika MUHAS

JUMLA ya miradi ya tafiti iliyopata ufadhili 135 inaendelea kufanyika katika Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) zikilenga kuzingati vipaumbele vya nchi vya kuwema mifumo imara ya afya ili kukabiliana na changamoto za afya zinazoibuka nchini na duniani.

Kaimu Makamu Mkuu wa MUHAS, Prof Apolnaly Kamwagwa amesema kongamano la kisayansi ni sehemu ya watafiti kupeleka tafiti,kuawasilisha na kujadili ili ziwafikie wananchi .

Amesema tafiti hizo zimewasaidia MUHAS kuwa ya kwanza kwa Afrika Mashariki na ya tano kwa bara la Afrika.

“Hizi tafiti zimelenga kutatua matatizo katika sekta ya elimu na afya mchango wa watafiti ni mkubwa ukienda kwenye huduma za afya sasa tunatoa wabobezi wa shahada ya tatu,Yanaleta mabadiliko na kuboresha huduma na mifumo ya afya na tunaangali ngazi za chini kama Zahanati ,kituo cha afya hadi hospitali ya Wilaya,”amesisitiza.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, James Mdoe amesema lengo la tafiti ni kutatua changamoto ambazo ziko katika jamii.

“Baada ya utafiti tunapata matokeo katika mikutano na matatizo ya afya ni yakiduni ambapo hapa pia wapo watafiti kutoka nje ya nchi wanajadiliana na mwisho kuja na maazimio na serikali tunapenda na tupo tayari kusaidia kufanyika kwa tafiti kwasababu bila tafiti hatuwezi kutatua changamoto na huwa changamoto zinabadilika kama vile Covid-19 na dawa zingine zinakuwa sugu,”ameeleza.

Mdoe amesema kuwa serikali ipo tayari kutoa usaidizi kama kujenga majengo ,maabara na mradi wa mageuzi ya kiuchumi unaojengwa Muhimbili ambapo zaidi Sh bilioni 100 zitatumika ndani ya miaka mitano hadi 2026.

“ Watajenga maabara mpya,madarasa,kusomesha wataalamu ,kubadilisha mitaala kuendana na hali halisi ,kujenga kampasi mpya ua Muhimbili huko Kigoma.

Amefafanua kuwa Serikali inawalea vijana wadogo kupitia mradi wa ufadhili wa ‘Samia Scholarship’ambao unatoa fedha kwaajili ya kusomesha wanafunzi wanaoingia kidato cha sita wanapoingia shahada ya kwanza kwa masomo ya sayansi.

Ameeleza kuwa Sasa kuna wanafunzo 640 wanasomeshwa kupitia ufadhili huo na watachukua tena wengine 640 wenye vipaji na kuwaingiza katika sayansi ili kutatua changamoto za jamii.

Habari Zifananazo

Back to top button