‘Miradi izingatie thamani ya fedha’

TANGA: KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Godfrey Mzava, ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe kusimamia ujenzi wa Zahanati ya Magila Gereza uweze kukamilika kwa wakati na kuzingatia thamani halisi ya fedha.

Maagizo hayo ameyatoa leo wakati mwenge huo ulipoweka jiwe la msingi katika mradi wa Zahanati ya Magila Gereza unaojengwa kwa nguvu za wananchi.

“Hakikisheni mradi huu unakamilika kwa wakati, katika viwango vyenye ubora ili wananchi waweze kupata huduma karibu na eneo lao, “amesema Mzava.

Akitoa taarifa ya mradi huo Mtendaji Kata hiyo, Catherine Rogers amesema kuwa mradi huo umegharimu kiasi cha Sh Mil 44 huku nguvu za wananchi zikiwa ni Sh Mil 19.

“Kutokana na uwepo wa changamoto ya umbali  kufuata huduma ya afya, ndipo wananchi walipoamua kuanzisha mradi huu kwa nguvu zao na walipofika kwenye lenta, Halmashauri waliongeza nguvu kwa kuchangia Sh Mil 25,”amesema Rogers.

Habari Zifananazo

Back to top button