Miradi mipya 240 yasajiliwa

WAZIRI wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji amesema katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Machi, 2023 wizara imesajili miradi mipya 240, ambapo kati ya miradi hiyo wazawa wanamiliki miradi 89, wageni miradi 94 na ubia miradi 57.

Akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024 bungeni jijini Dodoma, Dk Kijaji amesema jumla ya Dola milioni 4,387.17 zinatarajiwa kuwekezwa katika miradi hiyo ambayo itatengeneza ajira 39,245.

Habari Zifananazo

Back to top button