Miroshi awaangukia Watanzania

DAR ES SALAAM: Nyota wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa stars’, Novatus Dismas Miroshi amewaangukia wapenda soka akijutia kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa kusaka kucheza fainali za Kombe la Dunia mwaka 2026 dhidi ya timu ya taifa ya Morocco ambao Taifa Stars ilipoteza mabao 2-0.

Kupitia ukurusa wake wa Instagram Miroshi amesema licha ya kupoteza jana bado anaamini Tanzania ina nafasi ya kutamba katika michezo ijayo.

Advertisement

“Nipende kuwaomba radhi wapenda soka wote na Watanzania kwa kupata kadi nyekundu lakini bado tuna nafasi kubwa ya kufanya vizuri ‘’ ameandika Miroshi.

Kwa matokeo hayo ya jana Taifa Stars imesalia na alama zake tatu ikishika nafasi ya nne kwenye kundi E nyuma ya Morocco, Zambia na Niger wenye alama tatu pia.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *