Miss Tanga kufanyika Mei 6

SHINDANO la kumsaka Miss Tanga 2023 linatarajia kufanyika Mei 6, mwaka huu mkoani Tanga.

Akizungumza leo Machi 16, 2023 Dar es Salaam wakati wa uzinduzi rasmi wa shindano hilo, Mratibu wa shindano hilo, Victoria Martin amesema dirisha la kuchukua fomu za kuwania ulimbwende wa mkoa huo limefunguliwa leo na mwisho kwa wanaotaka kushiriki itakuwa Jumamosi Machi 18,2023.

“Dirisha la kuchukua fomu limezinduliwa rasmi leo na litafungwa Machi 18, 2023 huku usaili unatarajiwa kufanyika siku hiyo Tanga Beach Resort ,warembo watakaopatikana watanza mazoezi rasmi,” amesema na kuongeza kuwa mshiriki anatakiwa kuwa na umri wa miaka 18 hadi 24 na asiwe ameolewa wala kuwa na mtoto.

Habari Zifananazo

Back to top button