Miss Tanzania 2023 bado yupo yupo kwanza!

DAR ES SALAAM; “Mwana FA unaoa lini? (Bado nipo nipo kwanza)Unasema? (Bado nipo nipo sana)Mwana FA unaoa lini? (Bado nipo nipo mwana)Eeh? (Wa kuoa ntakuwa mimi mwana!?)

“Mwana FA unaoa lini? (Bado nipo nipo mama)Unasema? (Bado nipo nipo sana)Mwana FA unaoa lini? (Bado nipo nipo kwanza)Eeh! (Wa kuoa ntakuwa mimi mama!?),” huo ni wimbo Bado Nipo Nipo Kwanza wa msani Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA, ambaye sasa ni Mbunge wa Muheza na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Mwana FA alikuwa akizungumzia kuhusu ndoa, kwamba bado hajafikiria, sasa achana na Mwana FA, hebu mgeukie Miss Tanzania mwaka 2023, Halima Kopwe naye amekuja na staili kama ya Mwana FA, akidai kutokana na wingi wa kazi anazofanya muda wake ni mchache, hivyo hawezi kujihusisha na masuala ya mapenzi kwa sasa.

 

Halima amesema kwa sasa bado anaendelea na kazi zake, hivyo hatoweza kuingia katika mahusiano na yeyote hadi atakapomaliza kazi zake mwaka wowote.

“Muda mwingi nimekuwa katika project zangu na muda wa kuingia katika mahusiano kwa kuwa mahusiano yanataka muda, nami kwa sasa sina muda nipo single na nitaendelea na project zangu sitaki mapenzi,” amesema Halima na kongeza:

“Kwenye kubadilisha mawazo yangu mara nyingi nikijiona mpweke natoka na marafiki, wapo tunabadilisha mawazo na kufurahia maisha na kuwa sawa zaidi, “amesema mrembo huyo.

Habari Zifananazo

Back to top button