Kamati za maji vijiji, kata zijengewe uwezo

MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Projestus Tegamaisho wamewasilisha ombi maalumu kwa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) kuhakikisha kamati za kushughulikia malalamiko ngazi ya vijiji na kata zilizoundwa zinaongezewa uwezo wa kukabiliana na changamoto za walalamikaji.

Ombi hilo limetolewa kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa vyombo vya watoa huduma ya maji ngazi ya jamii CBWSO’s ulioandaliwa na RUWASA na kuwakutanisha wadau mbalimbali pamoja na madiwani, watendaji wa serikali, wahifadhi wa mazingira na kuongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Missenyi, Kanali Wilison Sakulo.

Tegamaisho alisema kuwa kwa sasa kunamabadiliko makubwa katika sekta ya maji na vijiji vingi vinapata maji kwa wakati hivyo kamati hizo zitapunguza adha ya wananchi ambao wangelipa nauli kuja mpaka wilayani kuleta malalamiko Yao , ambapo amewaomba viongozi wa RUWASA kuhakikisha wanawajengea uwezo wa kutosha katika kusikiliza kero na zile zenye uwezo wa kutatuliwa zitatuliwe kwangazi ya vijiji.

“Hakuna kipindi ambacho tumepata nguvu ya kuongoza kama madiwani na kuwa na furaha Kama kipindi hiki ambacho RUWASA wanafanya kazi Yao ipasavyo, ukiongolea maji katika Wilaya ya Missenyi ambayo haina historia ya kuwa na maji miaka mingi iliyopita unashukuru sana utendaji wa serikali, tunashukuru kwa kuunda vyombo vya malalamiko ambavyo vikije gewa uwezo vitafanya kazi nzuri kwa upande wa madiwani tunafurahia utendaji kazi”alisema Tegamaisho.

Taarifa ya mwaka iliyowasilishwa na Mratibu Redempta Bilindaya kutoka RUWASA Missenyi ilionyesha kuwa mpaka Sasa Wilaya ya Missenyi imeunda kamati za kushughulikia malalamiko 14 ngazi ya kata ,na kamati 44 ngazi ya vijiji.

 

Alisema kuwa Wizara ya Maji kupitia utekelezaji wa program ya huduma ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira kupitia ufadhili wa Benki ya Dunia kwa mwongozo wa kutekeleza kwa matokeo (PforR) imeonyesha hitaji la kuzingatia masuala ya kijamii na kimazingira kwa kuunda kamati hizo Jambo ambalo limetekelezeka katika wilaya ya Missenyi.

Meneja wa RUWASA wilayani Missenyi, Mhandisi Endrew kilembe alisema kuwa asilimia 78 ya wakazi wanaoishi katika wilaya ya Missenyi wanapata maji Safi na salama ambapo Wilaya hiyo inawakazi wapatao 245,395 na wakazi 191,407 wanapata maji.

 

Alitoa wito kwa viongozi ambao ni madiwani kusisitiza wananchi wao kulinda miundombinu ya maji,kuacha uvamizi katika vyanzo vya maji kutokapanda Miti isiyorafiki namazingira karibu na vyanzo vya maji pamoja na wananchi kuchangia huduma za maji Kama ulipaji wa bili kutokana na baadhi kutolipia bili kwa wakati .

Mkuu wa Wilaya ya Missenyi, Kanali William Sakulo ameendelea kusisitiza ulinzi wa vyanzo vya maji na miundo mbinu ya maji ili kuhakikisha miradi inayotekelezwa na serikali inadumu vizazi hadi vizazi .

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x