‘Miti shamba inaweza kusababisha ugumba’

WANAWAKE mkoani Tabora wameshauriwa kuacha kutumia dawa za mitishamba kwa ajili ya kupata watoto kwa sababu njia hizo zinaweza kusababisha wakapata ugumba na wasizae tena maishani.

Badala yake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Tabora ya Kitete, Dk Mnubi Baguma amewataka kuwaona wataalamu hospitalini wanapoona kuna shida ya kupata mtoto kwani kwa kutumia miti shamba wako hatarini kuharibu kila kitu.

Akizungumza na HabariLEO, Dk Baguma aliwataka wanawake wanaotafuta uzazi kwenda katika  zahanati, vituo vya afya na kwenye hospitali kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na ushauri wa kitaalamu na kitabibu na siyo kukimbilia kwa waganga wa jadi.

Alisema kwenye miti shamba, licha ya kuharibu kabisa uwezekano wa kupata watoto, miti shamba inaweza kuwaletea madhara mengine ikiwemo mingi kuhusishwa na kuharibu figo.

“Kama utakunywa dawa za asili zinazoathiri mji wa uzazi, uke, mirija, mayai au kuvuruga mtiririko wa hedhi matokeo yake ni kupata ugumba,” alisema Dk Baguma.

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button