Mitungi ya gesi kutolewa bure vijijini

JUMLA ya mitungi 100,000 inatarajiwa kutolewa bure ifikapo Mwezi Julai,2023  katika maeneo ya vijijini nchi nzima, ikiwa ni hatua ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi.

Mpango huo umekuja mara baada ya serikali kutenga kiasi cha Sh Bilioni 3.2 kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kwa ajili ya usambazaji wa gesi safi ya kupikia.

Mkurugenzi wa Uenezaji Masoko na Teknolojia Kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Advera Mwijage amesema hayo leo  jijini Dar es Salaam alipokutana na wadau wa gesi nchini na kueleza kuwa wameshaanza kuweka fomu ya maoni tangu Aprili 19  na kukamilishwa Mei,10,2023, ili kupata watu watakaonufaika na gesi hizo.

“Tumefanya kikao na wasambazaji wa mitungi ya gesi na kwa hapa Tanzania sasa tuna kampuni 11 na bahati nzuri wote wamefika na ujumbe wetu kwao ni wao kuwa tayari kushirikiana na serikali kuhakikisha kwamba tunasaidiana kwenye usambazaji wa nishati safi na salama maeneo ya vijijin,”ameeleza.

Amesema  nishati safi ni ile ambayo haichafui mazingiza, inalinda afya ya mwananchi,  lakini pia inatoa fursa kuwa kazi ya kupika ni starehe isiwe shida mtu anapika anatoa machozi.

Mwaijage alibainisha kuwa Serikali inamipango mingi kuhakikisha wananchi wote wanafikiwa na nishati hiyo na licha ya kufikiwa wakiihitaji wapate kwa wakati.

“Isiwe  kama sasa ukitaka huduma ya gesi iliyojaa kuna mtu anatembea kilometa 10 hadi 30 kama  mtu ana nia ya kuwa nayo kunakuwa na gharama tena ya kufuata sasa hizo ni changamoto ambazo tunatakiwa kutatua na hawa wasambazaji, ili watusaidie kusambaza huduma hizi maeneo ya vjijini ziwepo,”amesisitiza.

Amesema Mradi huo ni wa  mfano na kutoa elimu kwa ajili ya nishati ya gesi na kwa ajili ya kupikia, hivyo lengo ni kupeleka huduma na elimu kwa wananchi kwa lengo la kutoka kwenye kupikia mkaa,kuni ,mkaa mbadala na nishati nyingine ili watumie gesi.

Amesema pia wataongea na wenye majiko mbadala ambayo yanatumiwa gesi kidogo pia kusambaza  gesi asilimia maeneo ya Mtwara,Lindi, na Pwani

Habari Zifananazo

Back to top button