Miundombinu umwagiliaji mbegu mashamba ya ASA yazinduliwa

NAIBU Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde amezindua rasmi ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji katika mashamba ya uzalishaji mbegu yaliyo chini ya Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA).
Uzinduzi huo ni utekelezaji wa mpango wa serikali wa kuzalisha mbegu bora kipindi cha kiangazi ili kuondoa changamoto ya uhaba wa mbegu nchini.
Katika taarifa yake aliyoitoa leo Novemba 4, 2022 Kilosa mjini mkoani Morogoro, Mavunde amesema mradi huo utagharimu kiasi shilingi 18.
“Dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa Samia Suluhu Hassan ni kuondoa changamoto zinazomkabili mkulima, mojawapo ikiwa ni ya upatikanaji hafifu wa mbegu bora msimu wa kilimo.”Amesema na kuongeza
“Ndiyo maana, Rais ametuongezea fedha za bajeti ili tuweze kuweka miundombinu ya umwagiliaji kwenye mashamba ya mbegu ambayo itapelekea mbegu bora kuzalishwa kabla ya kuanza kwa msimu wa kilimo.”Amesema
Aidha, amesema visima vitano virefu vya maji vilivyochimbwa katika shamba hilo la ASA vitasaidia kuzalisha maji yatakayohifadhiwa katika bwawa lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita milioni 45.
Pia, Mavunde ameitaka ASA kushirikiana na sekta binafsi katika uzalishaji wa mbegu bora ili waweze kufikia lengo.
‘Ni lazima tuunganishe nguvu kwa pamoja baina ya serikali na sekta binafsi na kamwe hampaswi kuwa washindani bali mtegemeane kwa manufaa ya nchi.”Amessitiza
Mavunde, amemuagiza Mtendaji Mkuu wa ASA, Dkt. Sophia Killenga-Kashenge kuhakikisha mashamba yote ya ASA yanalimwa na kuongeza uzalishaji wa mbegu, badala ya kuyaacha kama mapori kama ilivyo sasa sambamba na kuwekewa uzio ili kuyalinda na uvamizi kutoka kwa watu mbalimbali ambao wanayaona kama hayatumiki.
Naye mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Alhaj Majid Mwanga aliishukuru Serikali kwa kupeleka mradi huo mkubwa Kilosa na kusisitiza kuwa wataendelea kushirikiana na ASA bega kwa bega ili m uweze kuleta tija kwa wananchi wa Kilosa na Tanzania kwa ujumla.