Mizengo Pinda achangia masomo ya vijana Mtwara

WAZIRI Mkuu mstaafu wa Tanzania, Mizengo Pinda anaadhimisha miaka 75 ya kuzaliwa kwake katika Mkoa wa Mtwara kwa kuchangia gharama za msomo kwa vijana ili waweze kupata elimu.

Akizungumza leo mkoani Mtwara kuhusu ujio huo wa Waziri Mkuu huyo mstaafu, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali, Ahmed Abbas amesema maadhimisho hayo yatafanyika Agosti 12, 2023 yatayoanza na misa takatifu majira ya saa 4 asubuhi katika Kanisa Kuu la watakatifu wote mkoani humo.

Aidha, zoezi hilo ni moja ya kuunga mkono kwa vitendo jitihada za mfuko wa kiuchungaji wa elimu mkoani humo wa Pastoral Education Fund (MPEF) kwenye jitihada ya kutafuta fedha kwa ajili ya ufadhili wa masomo kwa wanafunzi hao wahitaji nchini.

Misa hiyo itafuatiwa na jumuisho la uchangiaji (Harambee) itakayoanza majira ya saa 6:30 mchana katika viwanja vya kanisa hilo hivyo amewataka wananchi mkoani humo, nje ya mkoa huo na nje ya nchi kujitokeza kwa wingi kumuunga mkono waziri mstaafu huyo katika nia yake hiyo kubwa na ya kipekee ya kuchangisha fedha katika suala hilo la elimu.

Mfuko huo ulizinduliwa rasmi Januari 2021 ikiwa ni wazo la pamoja kati ya mkoa huo, Jimbo Katoliki Mkoa wa Mtwara na Chuo Kikuu cha Saut mkoani huo (Stemco) ikiwa serikali inaunga mkono jitihada hizo kubwa za kuhakikisha hakuna mtoto, kijana wa kitanzania mwenye changamoto hiyo ya kiuchumi anachwi nje ya fursa za kujiendeleza kielimu.

Aidha mpaka sasa idadi ya wanafunzi waliyofadhiliwa kwa mwaka wa taaluma 2021/22 ni 1064 kutoka mikoa yote 26 ya Tanzania Bara na mkoa mmoja kutoka Zanzibar na mwaka 2022/23 wamefadhiliwa wanafunzi 1128.

‘’Ninaomba wananchi wote tujumuike kwa pamoja siku ya tarehe 12, Agosti mwaka huu kwenye tukio hilo kubwa muhimu ndani ya mkoa wetu lakini pia kwa taifa kwa ujumla.”amesema Abbas

Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko huo, Padre Alex Masangu amesema kulikuwa na tafakari kubwa kuhusiana na vijana hao wenye changamoto hiyo kubwa ya kiuchumi kwamba nini kifanyike kutokana wapo vijana ambao wanakuja vyuoni wakiwa na hayo mazingira hivyo uongozi huo umepata maamuzi hayo baada ya kujionea na kubaini kuwepo kwa changamoto hiyo.

‘’Tukaona kwa nini tusifanya kitu ambacho kitaweza kuongeza nguvu kwa zile jitihada zilizopo na sisi kama chuo, uongozi kulitafakari kwa pamoja tukaamua kuanzisha hiki kitu au chombo ambacho kitatafuta fedha kwa ajili ya kutoa ufadhili wa masomo kwa vijana hao wenye changamoto kubwa kiuchumi’’,amesema Masangu

Habari Zifananazo

Back to top button