Mjane nyama ya swala aachiwa huru

JAJI Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Iringa, Elvin Mgeta amemuachia huru Maria Ngoda ambaye awali alihukumiwa kifungo cha miaka 22 jela kwa kosa la kukutwa na vipande 22 vya nyama ya swala.

Kwa kupitia uamuzi wa mahakama hiyo, Jaji Mgeta amesema kutokana na hoja zilizowasilishwa na mkata rufani Ngoda hana hatia na yupo huru.

Amesema rufaa hiyo iliyosimamiwa na Mawakili wa Chama cha Wanasheria Tangayika (TLS) Kanda ya Iringa ilikuwa na hoja 13 zilizoonesha mashtaka yaliyotolewa dhidi ya Ngoda hayakuthibitishwa na mahakama iliyotoa hukumu hiyo.

Maria alihukumiwa miaka 22 jela, Novemba 3, 2023 na Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa Said Mkasiwa.

Habari Zifananazo

Back to top button