Mama Janeth Magufuli atunukiwa tuzo

MJANE wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, hayati Dk John Magufuli, Mama Janeth Magufuli, ametunukiwa tuzo ya heshima ya kimataifa toleo la tatu, inayotolewa na taasisi ya Martha Tshisekedi Kasalu maarufu M. T. Kasalu, kutambua mchango wake kwa taifa la Tanzania na kwa hayati Magufuli akiwa Rais.
Tuzo hiyo hutolewa kwa wenza wa viongozi wakuu wa nchi na watu maarufu duniani kwa kutambua michango yao kwa wenza wao, jamii na Taifa husika.
Tuzo hiyo M. T. Kasalu, Femme D’Honneur Trophee, ilitolewa jana Ijumaa Machi 24, 2023 katika hoteli ya Pullman jijini Kinshasa.
Waandaaji wa tuzo hiyo ni Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Urithi ya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ( DRC) wakishirikiana na Taasisi ya Lizade