Mkalama waukubali moto wa Samia

KAMATI ya Fedha Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama ikiongozwa na mwenyekiti wa halmashauri hiyo, James Mkwega pamoja na Mkurugenzi Mtendaji, Asia Messos , imefanya ziara ya siku mbili kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali wilayani Mkalama.

Akizungumza kwa niaba ya mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Emmanuel Kabea ambaye ni makamu mwenyekiti wa halmashauri amemshukuru Rais, Dk Samia Suluhu Hassan kwa mazuri anayofanya ya kuleta maendeleo kwa wananchi pamoja na usimamizi mzuri unaofanywa na uongozi wa halmashauri wa kusimamia miradi inayotekelezwa na serikali wilayani Mkalama.

“Tunamshukuru sana Rais wetu Dk Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anaoifanya lakini pia tunaishukuru halmashauri na usimamizi wa Mwenyekiti James Mkwega kazi zinaenda vizuri,ushirikiano wake na Mkurugenzi pia ushirikiano wake na waheshimiwa madiwani” Emmanuel Kabea

 

Habari Zifananazo

Back to top button