Mkandarasi atakiwa kukamilisha mradi wa umeme kwa wakati

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme ameitaka kampuni Sinohydro Company Limited iliyopewa kandarasi ya kujenga mradi wa umeme wa Jua wenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 323 kukamilishwa kwa wakati.

Mndeme aliyasema hayo Jana alipokuwa akiongea na wadau pamoja na viongozi kutoka shirika la Umeme (TANESCO) na Wananchi waliopisha mradi huo kwenye kijiji cha Ngunga Wilaya ya Kishapu huku akieleza mradi huo utatekelezwa kwa kipindi cha miezi 17.

“Mkandarasi uliyepewa dhamana ya kujenga mradi huu mkubwa ninataka ukamilishwe kwa wakati na kwa kuzingatia muda, viwango, thamani na bajeti tuliyokubaliana ili wananchi waanze kunufaika na uwepo wa mradi huu,” alisema Mndeme.

Mndeme aliwakumbusha Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD group) – Dar es salaam Agency nakuwaeleza serikali inafanya kazi bega kwa bega, itawapatia ushirikiano wakati wote wa utekelezaji wa mradi.

Mndeme alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha mradi huu mkubwa wa umeme hasa kuja kutekelezwa katika kijiji hicho na wananchi wa eneo hilo watanufaika kwa kupata ajira.

“kutekelezwa kwa mradi huu kunakuja kuondoa kabisa changamoto za nishati ya umeme kuongeza ajira hasa kwa wananchi na kuimarisha uchumi wa wananchi wetu, na haya ndiyo malengo ya Rais”. alisema Mndeme.

Naibu mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo Ufaransa AFD Group Dar es salaam Agency Philippe Micheud lisema wao wameridhishwa na maandalizi yaliyowekwa katika kutekeleza mradi huu na wamevutiwa na eneo lilitengwa katika utekelezaji wake.

Meneja mradi wa umeme Jua Mhandisi Emmanuel Anderson alisema TANESCO wamejipanga vema katika kusimamia na kuhakikisha mradi huu unakamilika kwa wakati na kwa kiwango.

“Huu ni mradi wenye jumla ya megawati za umeme 150 ( MW 150 ) unaotekelezwa kwa awamu, ambapo kwa sasa awamu ya kwanza unaanza na megawati 50 na kisha kufuatiwa na megawati 100” alisema Anderson

Mradi huu unachukua eneo la zaidi ya hekari 1000 ambapo Wananchi 110 wamekwishapisha eneo hilo kwa kulipwa fidia na utekelezwaji wa mradi huu unafanywa na mkandarasi wa Kampuni ya Sinohydro CO. LTD.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x