Mkata umeme Msenegali atua Simba

Simba imemsajili kiungo mkabaji, Babacar Sarr (26) raia wa Senegal kwa mkataba wa miaka miwili akitokea US Monastir ya nchini Tunisia.

Taarifa ya usajili imethibitishwa kupitia mitandao ya kijamii ya klabu hiyo muda mfupi uliopita.

Sarr anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa Simba dirisha dogo baada ya Salehe Karabaka.

Advertisement