Mkataba uwekezaji bandari ni wa miaka 30

DODOMA; SERIKALI imeingia mkataba wa miaka 30 na Kampuni ya DP World ya kuendesha bandari ya Dar es Salaam.

Mikataba hiyo mitatu ya uwekezaji na uendeshaji wa bandari ya Dar es Salaam iliyoingiwa ni Mkataba wa Nchi Mwenyeji, Mikataba ya Ukodishaji na Uendeshaji wa Gati Namba 4 hadi 7 za bandari ya Dar es Salaam.

Aidha, Gati Namba 0 hadi 3 za bandari ya Dar es Salaam zitatumiwa kwa pamoja baina ya Kampuni ya DP World na Serikali kupitia TPA kwa ajili ya shughuli zingine za kibiashara na Serikali.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mbossa amesema mikataba utahusisha baadhi ya magati ya Bandari ya Dar es Salaam na sio maeneo yote ya Bandari ya Dar es Salaam na mikataba hii haihusishi bandari nyingine za mwambao na maziwa.

“Mtaba huu una ukomo wa miaka 30 na utakuwa ukirejewa kila baada ya miaka 5, ikiwa ni pamoja na kurejea mpango wa uwekezaji,” amesema Mbossa.

Amesema pia kutakuwa na kampuni ya uendeshaji ambayo TPA itamiliki hisa;  kuwekwa kwa viwango vya utendaji (key performance indicators), ambazo mwekezaji anapaswa kuvifikia.

Kwa upande wa watumishi wa sasa wa TPA, Mbossa amesema wamepewa nafasi ya kuchagua kubaki TPA au kuhamia kwa mwekezaji.

“Jukumu la ulinzi na usalama katika eneo lote la bandari na yaliyokodishwa kwa Kampuni DP World yataendelea kubaki serikalini; mwekezaji atalipa kodi na tozo zote za serikali kwa kuzingaia sheria za Tanzania, “amesema.

Amesema sheria za Tanzania zitatumika katika utekelezaji wa mikataba hii ikiwa ni pamoja na kutoa fursa za Watanzania kushiriki katika uwekezaji huu kupitia vifungu vya sheria vinavyolinda maudhui ya ndani ya nchi ni haki ya serikali kujiondoa katika mikataba hiyo imezingatiwa.

Mbossa amesema uwekezaji huo utakuwa na manufaa kwa serikali, ikiwemo ongezeko la ufanisi kwa huduma zitakazotolewa kwa meli na shehena hali itakayovutia meli nyingi zaidi na shehena kubwa ya mzigo itakayohudumiwa na Bandari ya Dar es Salaam.

Pia uboreshaji wa huduma za bandari kwa kupunguza muda wa kuchakata nyaraka kwa kutumia mifumo ya kisasa ya TEHAMA ya Bandari itakayofungamanishwa na wadau wote wa bandari, kuongezeka kwa mapato ya Serikali hususan ya ushuru wa forodha kufuatia ongezeko la shehena na meli pamoja na udhibiti wa udanganyifu kupitia mifumo ya kisasa ya bandari ikakayofungamanishwa na mifumo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Pia amesema kuiongezea uzoefu TPA na kuwajengea uwezo wafanyakazi na Watanzania katika uendeshaji wa bandari kwa viwango vya kimataifa, kuimarisha nafasi ya ushindani wa Bandari ya Dar es Salaam kikanda na kimataifa.

“Ajira kwa watumishi wa TPA na ajira mpya kwa Watanzania kufuatia kupanuka kwa wigo wa shughuli za uendeshaji wa bandari; kupungua kwa gharama za kusafirisha mizigo kupitia bandari ya Dar es Salaam;” amesema na kuongeza:

” Kuwepo kwa meli za moja kwa moja kutoka bara la Mashariki ya Kati kuja Tanzania ikilinganishwa na hivi sasa ambapo mizigo ya Tanzania huja kupitia nchi jirani;” amesema.

Pia manufaa mengine aliyotaja ni kuwa siku za kusafirisha mizigo kutoka Mashariki ya Kati na Mbali zitapungua kutoka siku 30 za sasa hadi siku zisizozidi 15.

Kuchochea ukuaji wa sekta nyingine za uchukuzi kama vile reli na barabara kufuatia ongezeko la shehena linalotakiwa kusafirishwa kutoka bandarini kwenda sehemu nyingine, na kuchagiza na kuchochea shughuli nyingine za kiuchumi kama vile kilimo, ufugaji, usafirishaji wa madini pamoja na biashara.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
LoraHenrick
LoraHenrick
1 month ago

I am earning $81,000 so Far this year working online and I am a full time college student and just working for 3 to 4 hours a day I’ve made such great money. I am thankful to my administrator, It’s’ really user friendly and I’m just so happy that I found out about this.
.
.
Detail Here—————————————————————->>>  http://Www.BizWork1.Com

Work AT Home
Work AT Home
1 month ago

Make extra profit every week… this is a great part-time job for everyone… best part about it is that you can work from your home and earn from $100-$2000 each week … start today and have your first payment at the end of the week. 

This Website➤—————➤ http://Www.Smartcash1.com

Last edited 1 month ago by Work AT Home
Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x