Mkazi Shinyanga aililia CCM kupotea kwa mumewe

MKAZI wa kijiji cha Tinde mkoani Shinyanga leo amekiomba Chama cha Mapinduzi (CCM) kumsaidia changamoto ya kutekwa kwa mume wake tangu mwaka 2021.

Akizungumza leo mkazi huyo ambaye jina lake halikufahamika mara moja, ameeleza kuwa mume wake alipotea alipokuwa Baraza la Ardhi la Kata alipokwenda kwa ajili ya usuluhisho wa mwisho.

Makonda alisema “Mbona Polisi mnawaonea sana watu maskini, mtu ametekwa miaka mitatu iliyopita, eneo lake limechukuliwa na mtuhumiwa mnayemjua na kujengwa kiwanda lakini hamchukui hatua yoyote'”.

Advertisement

“Basi kama mnashindwa kumtafuta mtu aliyetekwa, mmeshindwa hata kutenda haki kwa kumrudishia eneo lake ambalo Takukuru imethibitisha kwamba wanalimiki kihalali mjane wake?

Hapana msifanye hivyo.”