DAR ES SALAAM; Shabiki wa klabu ya Simba na Arsenal, Yahaya Bakari ameshinda Sh 140,503,890 baada ya kubashiri kwa usahihi matokeo ya ligi mbalimbali duniani kupitia mchezo wa Perfect 12 wa kampuni M-Bet Tanzania.
Licha ya kumzawadia mshindi huyo, M-Bet pia imezindua kampeni mpya ijulikanyo kwa jina la M-Bet Likes You ambayo itawawezesha washindi mbalimbali kushinda zawadi ya kushuhudia mchezo wa fainali wa mataifa ya Ulaya ‘Euro 2024’ nchini Ujerumani kuanzia Juni 14 mpaka Julai 14.
Mshindi huyo Bakari ambaye ni mkazi wa mkoa wa Singida, amesema kuwa amefurahi kutwaa kitita kikubwa cha fedha ambapo katika maisha yake hakuwa na mategemeo ya kukipata.
Amesema kuwa yeye ni mfanyabiashara mdogo na ushindi huo utamfanya kuongeza mtaji na kuwasomesha watoto wake.
“Mimi ni mfanyabiashara wakala wa huduma za kifedha kwa njia ya mitandao ya simu. Sikuwa na mtaji mkubwa, kupitia fedha ya M-Bet, nitawezza kukuza mtaji na vile vile kusomesha watoto wangu,” amesema Bakari.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Masoko wa M-Bet, Allen Mushi amempongeza Bakari kwa kuwa miongoni mwa mamilionea na kuwaomba Watanzania wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea kujaribu bahati yao kwa kubashiri na M-Bet.
Wakati huo, Kampuni hiyo imezidua kampeni mpya ijulikanayo kwa jina la M-Bet Likes You ambapo zawadi kubwa ni kushinda tiketi ya kushuhudia fainali ya michuano ya Mataifa ya Ulaya iliyopangwa kuanza Juni 14 na kumalizika Julai 14 nchini Ujerumani.