Mke auawa kwa kuchomwa na vitu vyenye ncha kali

Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Ally Kitumbu, Geita

MWANAMKE aitwaye Amina Hassan (34) mkazi wa mtaa wa Lukirini (Mkoani) kata ya Kalangalala mjini Geita amefariki dunia baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu za tumboni, ubavuni na mkononi.

Marehemu, Amina Hassan (34)

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Ally Kitumbu amethibitisha taarifa hiyo na kumtaja mtuhumiwa wa tukio hilo ni mme wa marehemu aitwaye Mashaka Jeremia.

ACP Kitumbu amesema mtuhumiwa alitenda kosa hilo mnamo tarehe 30, Agosti mwaka huu majira ya saa tano usiku maeneo ya nyumbani kwao mtaa wa Lukirini, chanzo kikidaiwa kuwa ni mgogoro wa familia.

Advertisement

“Wakati Mashaka anatenda tukio hili, mtoto wao aitwaye Deborah Mashaka (15), mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Mujumuzi alishuhudia na kueleza baada ya tukio Mashaka alikimbia kusikojulikana.

Amesema baada ya tukio majirani walisaidia kuokoa maisha ya Amina ambapo walimpeleka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita na kwa bahati mbaya Septemba mosi mwaka huu, majira ya saa saba mchana alifariki dunia.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita, Mfaume Salum amekiri marehemu alipokelewa katika idara ya dharura akiwa na majeraha sehemu mbsalimbali za mwili yakionekana kusababishwa na kitu chenye ncha kali.

“Tulimpeleka chumba cha upasuaji kupata huduma ya haraka ya upasuaji na kugundua shida ambayio imeweza kutokea ndani ya mwili na alifanyiwa upasuaji usiku huohuo lakini baada ya kutoka chumba cha upasuaji ndani ya masa 20 alifariki dunia.”

Mwenyekiti wa Mtaa wa Mkoani mjini Geita, Salvatory Paulo amesema kabla ya tukio hilo wanafamilia hao walikuwa na mgogoro uliotokana na mke wake kuuza aridhi ya familia bila taarifa kwa madai ya kupata hela ya ada ya mtoto.

Amesema wakati mauzo ya aridhi ya familia yanatokea mme alikuwa kwenye shughuli zake za uchimbaji na alifuatilia na baadaye kutoa taarifa amesamehe suala hilo na kuamua kuweka kizuizi cha mauzo ya aridhi nyingine ya familia kwa njia ya barua ofisi ya mtaa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *