Mke wa Askofu ajinyonga kwa kuugua muda mrefu

GEITA. Biharamulo. Mke wa Baba Askofu Vitalis Sunzu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Biharamulo, Monica Vitalis (45) amekutwa amefariki dunia kwa kujinyonga kando ya aneo la hifadhi ya Taifa ya Burigi Chato.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Safia Jongo amethibitisha kwa waandishi wa habari mjini Geita na kueleza mwili wa marehemu ulionekana Novemba 8, 2023.

Kamanda amesema uchunguzi wa Jeshi la Polisi kwa ushirikiano na madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (CZRH), umebaini chanzo ni msongo wa mawazo kwa marehemu kutokana na ugonjwa wa muda mrefu.

Advertisement

Amesema jeshi la polisi lilipokea taarifa za tukio hilo siku ya Novemba 8, 2023, majira ya saa tisa mchana zikieleza mwili wa marehemu ulikutwa ukining’inia kando ya hifadhi katika kijiji na kata ya Kasenga wilayani Chato.

“Baada ya kupata taarifa hizo timu ya upelelezi ilienda pale na kukuta ule mwili ukiwa unaning’inia juu ya mti akiwa amejinyonga na kamba ya manila, kwa hiyo mwili ule ulifanyiwa uchunguzi pale eneo la tukio,” amesema Kamanda Jongo.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *