Mkemia: Hakuna dereva anayepoteza maisha kwa kemikali

OFISI ya Mkemia Mkuu wa Serikali na wasafirishaji wa kemikali wamesema hakuna dereva anayepoteza maisha kwa kuathiriwa na kemikali kutokana na uhifadhi usiofaa wakati wakusafirisha.

Ufafanuzi huo umetolewa Mara baada ya kusambaa kwa video katika mitandao ya kijamii iliyorekodiwa na raia wa nchi jirani akishutumu usafirishaji usiofaa kwa kemikali hapa nchini ambapo alidai madereva wanaosafirisha kemikali hizo kupoteza maisha kutokana na athari za usafirishaji usio salama.

Mtu huyo anasema wao nchini kwao gari ambayo imebabe sumu yenye alama ya fuvu la mtu kitaalamu hiyo ni kemikali ya sumu hivyo zinasafirishwa kwa msafara wa gari 20 hadi 30 na zinakuwa na wataalamu magari madogo mawili wanakuwa kwenye hivyo gari lakini anashangaa Tanzania kasha la sumu linasafirishwa wazi.

Advertisement

Tuhuma za pili ni wataalamu wakusafirisha watanakiwa kutengewa sehemu Tanzania hawatengewi na akawashauri wataalamu wa afya na Akatoa taarifa kila wiki anakufa dereva Kule Tunduma na wenye kampuni hawafatilii na hawajali.

Wakizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam walisema sheria zote za kusafirisha kemikali zinazingatiwa hapa nchi kulingana na aina ya kemikali.

Mkurugenzi wa Huduma za Udhibiti wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Daniel Ndiyo amesema kwa mujibu wa kanuni ili msafirishaji asafirishe lazima aweze kusajiliwa na sifa za anayeomba zinazingatiwaa kama anauwezo na kuwa na wataalamu wakutosha,vifaa vyakujikinga na kukabiliana na dharura.

Taratibu zingine alizoainisha ni magari lazima yawe sahihi na yenye sifa kulingana na Kemikali inayosafirishwa kulingana na hali ya usalama, kutoa elimu kwa wafanyakazi katika kuhifadhi au kusafirisha wasafirisha na Dereva anayesafirisha kemikali lazima awe amepata mafunzo na anaposafirisha lazima awe na kadi ya usalama ikiwa ni pamoja na yeye kujikinga inapotokea ajali.

“Tumetoa maelekezo unaposafirisha kemikali hatarishi hasa za migodini ni lazima isafirishwe kwa magari yasiyozodi 10 hapa kuna magari mawili madogo moja mbele na nyingine nyuma yanabeba wataalamu na dawa tiba kama mtu akidhurika au ajali dawa tiba inafifisha,”amesisitiza.

Ndiyo amesema katika magari hayo lazima yawekwe alama mahususi kulingana na Kemikali iliyobeba lengo kuwaambia watu ikitokea ajali wasikaribie na mengine yanakemikali zinazolipuka.

“Tukiona masharti ya ziada yanahitajika kwa aina ya kemikali tunaweka mfano vilipuzi migodini mkemia ataweka masharti ya ziada kwa kushirikiana na polisi gari litasindikizwa

Amefafanua kuwa zipo kemikali za sumu ambazo haziruhusiwi kufungua mpaka pale zinapofika sehemu maalum ambazo zinatumika na kuna zingine zinaweza kufunguliwa kulingana na maelekezo maalum kwasababu zinahitaji hewa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *